Miongozo ya Jumuiya

Miongozo yetu na Sheria na Masharti ziko hapa kuhakikisha ya kwamba kila mteja anafurahia Hot or Not kwa usalama na uwajibikaji.

Mambo yanayoruhusiwa Hot or Not

Tafadhali pakia picha zako tu na video

Suala la hakimiliki ni zito sana kwetu. Kama hauna haki ya kumiliki picha au video, tafadhali usiibandike, kwani ni dhidi ya sharia zetu na unaweza kutolewa Hot or Not.

Heshimu wateja wengine

Sisi ni jumuiya tofauti sana. Hii inamaanisha kwamba unatakiwa uheshimu imani za wengine, vinavyowavutia na mali zao wakati unapokuwa kwenye Hot or Not.

Watumie wengine ujumbe uliouandika wewe mwenyewe

Kuliko kunukuu na kubandika ujumbe huo huo kwa wote uwapendao, soma wasifu wao. angalia wanapenda nini na time ujumbe unaofaa. 'Mambo, naona unapenda kuogelea' ni afadhali kuliko 'Mambo Mrembo!'

Fuatilia maagizo yetu

Hatupendi kukumbusha watumiaji wetu kufuata taratibu hizi, na tunachukia kuwazuia watu, basi cheza vizuri na utafurahia zaidi kwenye Hot or Not!

Shea maisha yako na wengine duniani

Hot or Not hukuwezesha kuitangazia dunia kuhusu wewe mwenyewe na kazi yako. Faidika na nafasi hii kujionyesha katika jumuiya yetu nzuri.

Starehe

Furahia muda wako kwenye Hot or Not. Zungumza na watu, jenga urafiki na panga kukutana na watu kiukweli. Lolote utakalofanya, usisahau kujivinjari!

Mambo yanayokatazwa Hot or Not

Usiwatukane matusi wengine

Jiheshimu unapokuwa Hot or Not kama unavyojiheshimu kwa kawaida katika maisha yako. Uwe mtu mzuri kwa watu unaokutana nao katika mtandao, kama unavyofanya ukikutana nao uso kwa uso.

Usijidai wewe ni mtu mwingine

Tunategemea kwamba utakutana na watu wa kweli kwa kupitia Hot or Not, kwa hivyo tunakuomba utumie jina lako la kweli, picha na taarifa katika wasifu wako. usijidai kuwa mtu mwingine au kutengeneza wasifu kama wanandoa au watu wawili au pia kama kikundi.

Usibandike maelezo yako ya kuwasiliana hadharani

Tafadhali usibandike namba yako ya simu, anwani, barua pepe au URL ya tovuti katika wasifu wako, picha zako au katika maoni unayoyaandika mbele ya hadhara kwani tutafuta picha hizo au maelezo hayo.

Usipakie mada zisizofurahisha na zenye ngono

Zipo sehemu ambazo unaweza kuenda na kupakia picha za ngono na zenye kushtusha, pia video, lakini hii si sehemu hiyo, kwa hivyo tafadhali usifanye hivyo. Hii haina maana ya kuwa huna ruhusa ya kuvutia katika picha zako, bali ni lazima uifahamu mipaka tu.

Usifanye mambo yoyote ya haramu katika tovuti yetu

Hatupendezewi na shughuli za haramu katika Hot or Not, ni hakika kwamba utafukuzwa kutoka katika tovuti, na ukashitakiwa serikalini.

Usitume takataka kwa wateja wetu

Usijaribu kuuza bidhaa, tovuti zingine au kujiuza katika Hot or Not. Utapigwa marufuku hapo hapo.

Usibandike picha za watoto wako

Ingawa umeachiwa uwanja kuwaambia watumiaji wengine kwamba una watoto katika chat au wasifu wako, hakura ruhusa katika Hot or Not kubandika picha za watoto, haa kama wewe mwenyewe umo ndani ya picha.

Kama hufuati miongozo hii, utapokea onyo (isipokuwa kama ni kwa jambo ambalo tunalikataza moja kwa moja). Kama hutazingatia onyo hili, basi utaweza kupoteza akaunti yako. Miongozo hii imetayarishwa kufanya Hot or Not pawe sehemu ya kirafiki na salama kwa watumiaji wote, hivyo tafadhali zingatia hili unapotumia tovuti.